ALII - African Leadership Initiatives for Impact

HakiElimu Opening Statement at the NextGen Leaders Fellowship

HakiElimu Representative

HakiElimu Representative speaking at ceremony

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Balozi wa Ireland,
Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani,
Mwakilishi wa Norwegian Church Aid,
Wageni waalikwa, vijana, mabibi na mabwana,

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee!

HakiElimu, kama mratibu mwenza wa programu hii muhimu, tungependa kuungana na wengine kuwakaribisha na kuwapongeza kwa dhati vijana hawa mia moja waliochaguliwa kuwa sehemu ya kundi la kwanza (cohort 1) la Jukwaa hili la Kuwajengea Uwezo wa Uongozi Vijana waliohitimu Kidato cha Sita. Hongereni sana!

"Samaki mkunje angali mbichi." - Swahili proverb meaning it's best to shape young minds early

HakiElimu inajivunia kuwa sehemu ya jukwaa hili muhimu la kujenga viongozi wa baadaye. Vijana hawa wamehitimu kidato cha sita kutoka shule mbalimbali za Tanzania Bara na Visiwani. Kwa takribani miaka 23 sasa, HakiElimu imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uzalishaji wa raia wenye fikra makini na mchango chanya kwa taifa lao kupitia elimu.

Sote tunafahamu umuhimu wa uongozi katika maendeleo ya aina yoyote na ustawi wa jamii. Ni wazi kuwa, pamoja na sababu nyingine, nchi zilizoendelea zimefanikiwa kutokana na aina ya uongozi wake, na zile ambazo bado ziko nyuma, zimechangiwa pia na aina ya viongozi wake.

The Importance of Youth Leadership

Leaders carry the vision and direction of families, institutions, communities, or nations. This fellowship for building leaders is crucial for the youth themselves and for the nation as a whole. This platform brings uniqueness by recognizing leadership talents at this early stage and nurturing them through training and mentoring.

Jukwaa hili pia, linatambua maeneo vipaumbele vya vijana hawa ili kuwaandaa kuwa viongozi katika sekta au taaluma wazipendazo. Ni wazi, katika dunia hii inayobadilika kwa kasi na yenye mwingiliano mkubwa, ushindani wa hiari na usiokuwa wa hiari kati ya mataifa duniani juu ya maendeleo na ustawi wa mataifa na watu wao haupingiki.

"Basi tunawaomba vijana, ninyi kama sehemu ya kwanza ya programu hii ambayo itakuwa na mwendelezo, kuzingatia mafunzo na kuyaishi katika kila ngazi ya maisha yenu. Tunatarajia kuziona nyota zenu za uongozi ziking'aa vyuoni, katika biashara, mashambani, na makazini mtakakokwenda hapo baadaye."

Ni matumaini yetu, mtakuwa mabalozi wazuri wa jukwaa hili na kama ilivyo kwa vijana hawa wa ALII, mtakuwa sehemu ya wanafunzi wa zamani (Alumni) wa NEXT GEN na mtachangia katika kuzalisha na kuwalea vijana wenzetu watakaokuja nyuma yenu hata baadaye.

Asanteni sana. Tunawatakia kila la kheri washiriki wote.